Numbers 15:32-36

32 aWaisraeli walipokuwa jangwani, mtu mmoja alikutwa akikusanya kuni siku ya Sabato. 33Wale waliomkuta akikusanya kuni wakamleta kwa Musa, Haruni na kusanyiko lote, 34 bnao wakamweka kifungoni, kwa sababu haikufahamika kwa wazi kwamba afanyiwe nini. 35 cNdipo Bwana akamwambia Musa, “Huyo mtu ni lazima afe. Kusanyiko lote lazima limpige mawe nje ya kambi.” 36 dHivyo kusanyiko likamtoa nje ya kambi na kumpiga mawe hadi akafa, kama Bwana alivyomwamuru Musa.

Vifundo Kwenye Mavazi

Copyright information for SwhKC